Numbers 3:1-6

Walawi

1 aHii ni hesabu ya jamaa ya Haruni na Musa kwa wakati ambao Bwana alizungumza na Musa katika Mlima Sinai.

2 bMajina ya wana wa Haruni yalikuwa: Nadabu mzaliwa wa kwanza na Abihu, Eleazari na Ithamari. 3 cHayo yalikuwa majina ya wana wa Haruni, makuhani wapakwa mafuta, waliokuwa wamesimikwa kuhudumu kama makuhani. 4 dHata hivyo Nadabu na Abihu walikufa mbele za Bwana walipotoa sadaka kwa moto usioruhusiwa mbele zake katika Jangwa la Sinai. Hawakuwa na wana; kwa hiyo Eleazari na Ithamari walihudumu peke yao kama makuhani wakati wote wa maisha ya Haruni baba yao.

5Bwana akamwambia Musa, 6 e“Walete watu wa kabila la Lawi mbele ya Haruni kuhani ili wamsaidie.
Copyright information for SwhKC